Monday, July 19, 2021
ADELE KWENYE PENZI JIPYA NA WAKALA WA LEBRON JAMES `RICH PAUL`.
Baada ya kukaa muda mrefu bila kuweka wazi mahusiano yake, hatimaye zoezi hilo limekuwa gumu kwa hitmaker wa ngoma ya "Hello", mrembo #Adele.
Adele alionekana kwenye viwanja vya basketball akifuatilia mchezo kati ya timu ya Phoenix Suns dhidi ya Milwaukee Bucks siku ya Jumamosi akiwa na mpenzi wake mpya Rich Paul, ambae ni wakala wa mchezaji LeBron James.
#Adele ambae ana mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 8, amemaliza kufuatilia talaka yake na aliyekuwa mume wake, Simon Konecki, mapema mwaka huu na hivyo kumpa nafasi Rich Paul kuchukua 'jimbo' hilo.
Wapo wanaounganisha matukio kati ya upendo alionao Adele juu ya mchezo wa mpira wa kikapu, kuhusishwa kwa kiasi kikubwa na mahusiano yake ya sasa na wakala Rich Paul.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment