Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Monday, July 19, 2021

WABUNGE WA VITI MAALUMU WAUNGA MKONO TOZO ZA MIAMALA.


 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amewataka Watanzania nchini kumuunga mkono Rais @SuluhuSamia kwa kuwa wazalendo katika kulipa kodi kwani uimara na ukuaji wa Taifa lolote kiuchumi hutokana na ulipaji wa kodi.


"Bila kumuunga mkono Rais Samia katika ukusanyaji wa kodi hatuwezi kumsaidia kuendesha Nchi, hizi fedha zinazotokana na makato haya siyo faida tu kwa Serikali bali ni kwetu sisi wananchi.

Tumuunge mkono Rais @SuluhuSamia katika ukusanyaji wa kodi za miamala kwani itasaidia kuirudisha Nchi yetu katika uchumi imara,tukumbuke wakati Rais alitueleza wazi kuwa uchumi wetu umeshuka kutoka asilimia 6.9 hadi 4.7 kutokana na athari ya janga la Corona," amesema Mariam Ditopile

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates