Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, September 28, 2021

BENKI YA NMB YADHAMINI MKUTANO MKUU WA ALAT KWA SH. MIL. 150.


 Benki ya NMB imedhamini Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kwa Sh. Mil. 150, huku ikijivunia makusanyo ya zaidi ya Sh. Trilioni 6 kupitia Mfumo wa Ukusanyaji Mapato ya Serikali Kielektroniki (GePG) katika kipindi cha miaka mitatu iliyoishia Julai 2021.

Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi ALAT Taifa umefanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo, ukifunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliyeambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai na Waziri wa Nchi Ofisi ya RaisTawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB (CEO), Ruth Zaipuna, alisema wanajivunia ushirikiano wao na ALAT, ambao umekuwa chachu ya kudhamini mara kwa mara mikutano yao hiyo na kuwa anaamini Jumuiya hiyo itauenzi uhusiano huo, huku wakiendelea kuifanya NMB kuwa benki namba moja katika Makusanyo ya Halmashauri zote nchini.


“Matarajio yetu ni kuendeleza uhusiano mwema kati ya ALAT na NMB, pamoja na ushirikiano mzuri na Halmashauri zote katika kukamilisha miradi mikubwa inayosimamiwa na Halmashauri zetu, lakini pia tumekuwa vinara wa makusanyo ya fedha za Serikali.

“Katika miaka mitatu iliyopita tumekusanya takribani Sh. Trilioni 6 kupitia Mfumo wa Ukusanyaji Mapato ya Serikali Kielektroniki (GePG), huku tukiwa sehemu ya ufanikishaji wa miradi na uendelezaji wa mazao ya kimkakati kote nchini,” alisema CEO Zaipuna.

Akifungua Mkutano huo, Rais Samia aliipongeza NMB kwa kubeba dhamana kufanikisha Uchaguzi wa ALAT Taifa, huku akiwataka Wajumbe kuchagua viongozi sahihi, ili kuitendea haki kaulimbiu ya mkutano huo isemayo ‘Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu,’ kwani ALAT imara ndio Msingi mkuu wa maendeleo endelevu yanayochakatwa

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates