Msanii maarufu nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele 'Steve Nyerere' ameteuliwa kuwa Balozi wa harakati za kupambana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (Uviko 19).Steve ameteuliwa leo Alhamisi, Agosti 12, 2021 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima jijini Dar es Salaam.
steve pamoja na wengine walioteuliwa ni Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini, Joyce Kiria na Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Lugangira.
Tangu janga la Uviko 19 liibuke tena nchini mwaka huu, Steve ameonyesha kupambana na janga hilo huku akihamasisha watu kupata chanjo ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huo hatari duniani.

0 comments:
Post a Comment