Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Friday, August 13, 2021

SERIKALI IMEWATAKA VIJANA KUJIFUNZA SOMO LA KUJIAJIRI.

  




SERIKALI imeendelea kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili Vijana nchini ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kufungua fursa zaidi kama vile fursa za ajira, mitaji na kutengeneza mazingira wezeshi na jumuishi yatakayowasaidia kushiriki kikamilifu kwenye nafasi mbalimbali za Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii.

 
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi alipokutana na Waandishi wa Habari katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana (International Youth Day) Agosti 12, 2021 kwenye Ukumbi wa Mkutano uliopo PSSSF, Jijini Dodoma.  
 
Alieleza kuwa, Serikali inaungana na Jumuiya ya kimataifa katika kuthamini mchango wa Vijana katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii kutokana na kushiriki kwao kikamilifu katika shughuli za Maendeleo ya Kiuchumi, kisiasa na kijamii.

“Dhumuni kuu la kuadhimisha siku hii ni kuiwezesha Jumuiya ya Kimataifa na jamii kwa ujumla kupata fursa ya pamoja ya kusherehekea na kutambua nafasi ya Vijana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Nchi zao.  Hii inatokana na ukweli kwamba vijana ndio kundi kubwa katika jamii yoyote na Vijana ndio wenye nguvu zaidi za kufanya kazi, Vijana ni wabunifu, Vijana ndio chachu ya mabadiliko chanya katika jamii na Vijana ndio warithi wa Mataifa yao,” alieleza Naibu Waziri Katambi

Katika kuthamini mchango wa vijana kuelekea siku hiyo Serikali imeendelea kuweka mifumo imara ya kitaasisi na kisheria inayowapa vijana fursa pana ya kushiriki katika kazi za maendeleo kwa ari na ubunifu mkubwa.

Alifafanua kuwa makadirio ya utafiti wa nguvu kazi (ILFS), idadi ya watu walio katika ajira imeongezeka kutoka watu milioni 20 mwaka 2014 na kufikia milioni 22.6 mwaka 2020. Ongezeko hilo limetokana na utayari na ushiriki mkubwa wa vijana kufanya kazi katika sekta binafsi.

“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhesimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuwawezesha vijana kujiendeleza kupitia ubunifu ambapo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali katika jamii lakini pia vijana wamekuwa wakihimizwa kutumia Ubunifu wao kujiajiri,” alisema

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates