Kutoka nchini Afrika Kusini Kampuni ya Samsung imezima TV zote zilizoibiwa wakati wa ghasia za uporaji mwezi Julai, na kuzifanya zisiweze kufanya kazi tena.
Ambapo kampuni hiyo imeweka wazi juu ya kuweka zuio hilo.
TV hizo zinaweza kufanya kazi endapo mtumiaji wa runinga iliyoibiwa anatumia mawasiliano ya intaneti kinyume na sheria, kwa mujibu wa Samsung.
Mfumo huo umetumia namba za usajili wa TV zote zilizoporwa kabla ya kuzuia matumizi yake.
Afrika Kusini ilikuwa na maandamano ya ghasia na kwa wiki kadhaa mwezi uliopita na yaliyosababisha watu zaidi ya 300 kuuawa na mali zenye zaidi ya thamani ya mabilioni ya randi kuharibiwa au kuporwa

0 comments:
Post a Comment