Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Thursday, August 26, 2021

RC MAKALLA KUANZA RASMI ZIARA YA UTATUZI WA MIGOGORO YA WANANCHI JIMBO KWA JIMBO.

 


 Ni sehemu mkakati wake wa *kuwafikishia wananchi msaada wa kisheria kwenye maeneo yao.*


- Awaalika *Wenye Migogoro kuwasilisha kero zao.*

- Asema *kila mmoja atapata haki yake kwa mujibu wa Sheria.*

- Awaandaa *wataalamu wa sekta mbalimbali kwaajili ya kuhudumia kila atakaefika.*

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* anatarajiwa kuanza rasmi *ziara ya kusikiliza na kutatua kero na changamoto za Wananchi* wa Mkoa huo Jimbo kwa Jimbo ikiwa ni Mpango wake wa kupatia *ufumbuzi kero za Wananchi.*

*RC Makalla* amesema ziara hiyo itaanza rasmi *Jumatatu ya August 30* kwenye *Jimbo la Kawe Viwanja vya Tanganyika Packers*, August 31 *Jimbo la Kibamba*, September 01 *Jimbo la Segerea,* September 02 *Jimbo la Mbagala* na September 03 *Jimbo la Kigamboni* ambapo zoezi litaanza kuanzia *Saa mbili Asubuhi Hadi majira ya jioni.*

Aidha *RC Makalla* amesema kutakuwa na *jopo la Wataalamu wabobezi* wakiwemo *Watendaji wa Serikali, Wanasheria, Kamishina wa Ardhi, Maafisa Ardhi, Jeshi la Polisi, TAKUKURU na Wadau wote* wanaojihusisha na masuala ya kisheria.

Pamoja na hayo *RC Makalla* ametoa *wito kwa Wananchi* wote Wenye Migogoro kutumia Fursa hiyo *kuwasilisha Malalamiko yao ili yaweze kupatiwa ufumbuzi kwa mujibu wa Sheria.*

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates