Ubalozi wa Russia Nchini Afghanistan umesema Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan aliondoka na mamilioni ya dola siku ya Jumapili wakati akiikimbia Nchi hiyo baada ya Wanamgambo wa Taliban kuingia kwenye Mji Mkuu wa Kabul, nae Balozi wa Afghanistan Nchini Tajikistan amepigilia msumari kauli hii kwa kusema Rais huyo ameondoka na dola milioni 169 za Kimarekani.
Balozi huyo aliyepo Tajikistan amesema pesa alizochukua Ghani ni mali ya umma hivyo Polisi wa kimataifa wanatakiwa kumkamata, vilevile Ubalozi wa Russia Nchini Afghanistan umesema pamoja na pesa nyingi alizochukua mpaka nyingine akashindwa kuzibeba kwa kukosa nafasi, aliondoka pia na Helikopta moja na magari manne.
Hata hivyo Ghani ambae leo Umoja wa Falme za Kiarabu umethibitisha kumpokea, amekanusha madai hayo ya kukimbia na pesa kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusisitiza kwamba ni madai ya uongo na uchonganishi na alifanya kukimbia Nchi ili kuepusha umwajikaji wa damu na msuguano.
0 comments:
Post a Comment