Wednesday, August 18, 2021
MWIMBAJI ANDERSON PAAK AMEACHA WOSIA KABLA YA KUONDOKA DUNIANI.
Mwimbaji Anderson .Paak ameamua kuacha wosia kabla ya Kuondoka duniani, wosia huo ameuandika kwenye mkono wake wa kulia ambapo umeeleza kwamba, haitaji mtu yeyote kuachia nyimbo zake baada ya kufariki dunia. Tangu miaka ya 90, imekuwa kama desturi kwa msanii akifariki dunia basi kazi zake ambazo hakuwa amezitoa, huachiwa kwa mfumo wa album au singles (posthumous album/singles), Anderson .Paak ameandika-
"Nikifariki dunia, tafadhali msiachie album au nyimbo zikiambatana na jina langu. Hizo zilikuwa kazi ambazo hazijakamilika (demos) na sikukusudia zisikike kwenye hadhira" - inasomeka tattoo hiyo.
Hivi karibuni tumeshuhudia wasanii waliofariki wakifanya vizuri sana kwenye mauzo ya kazi zao, Mac Miller, Pop Smoke, Juice Wrld, Prince na hata mwimbaji Aaliyah ambaye album yake iliachiwa baada ya kufariki dunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment