Kwa mujibu wa Tovuti ya Mercado Libre, kitambaa kilichotumiwa na mshambuliaji nyota wa zamani wa FC Barcelona ambaye kwa sasa ni mchezaji mpya wa Klabu ya PSG, Lionel Messi kufutia machozi, kipo sokoni na kinauzwa kwa shilingi bilion 2.3 za Kitanzania.
Bidhaa hiyo (kitambaa) iliyobeba machozi ya mchezaji huyo bora mara 6 duniani wakati akiiaga timu yake kuelekea PSG, imeelezwa kuwa kipo katika hali nzuri tu na kama utakua na Dola za Kimarekani milioni 1 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 2.3 za Kitanzania, basi utakipata kitambaa hicho.

0 comments:
Post a Comment