Saturday, August 28, 2021
BEYONCE ACHUKIZWA NA CHENI YENYE BLOOD DIAMOND.
Beyonce amechukizwa na kitenda cha kuvalishwa Almasi ya Tiffany Yellow ambayo ni miongoni mwa Almasi kubwa zaidi duniani kuwahi kuchimbwa bila kujulishwa historia ya Jiwe hilo. Beyonce alipiga picha na almasi hio shingoni na baadae kukosolewa kuwa amevaa 'Blood Diamonds' kutokana na hali ya wachimbaji na walivyoteswa na wakoloni wakati wanachimba Almasi hio.-
Almasi hii ilichimbwa nchini Afrika Kusini mnamo 1877, ina karati 128, Beyonce ni mtu wa kwanza mweusi kuvaa almasi hio. Mwigizaji wa Ghana anaeishi Marekani Karen Attiah aliandika, "Almasi hii ilichimbwa chini ya hali mbaya, wafanyikazi waliteswa na wakoloni na kupelekea kuwa na Ubaguzi wa rangi, kama mafanikio ya mtu mweusi ni kulipwa ili kuvaa Almasi yenye damu za watu basi bado tuko chini sana".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment