Friday, August 13, 2021
ALIFANYA UPASUAJI ILI AFANANE NA PAKA KUMFURAHISHA MUMEWE.
Kuna matukio mengine ukisimuliwa lazima utakataa kwamba halijawahi kutokea, lakini mengine ukakubaliana nayo baada ya kushuhudia picha au video.
Mwanamke mmoja ambaye ni sosholaiti kwenye mitandao ya kijamii, Jocelyn Wildenstein, anatajwa na Kitabu cha Kumbukumbu za Dunia kuwa enzi za ujana wake alifanya upasuaji katika uso wake uliomgharimu kiasi cha shilingi bilioni 5 za Kitanzania ili tu afanane na mnyama paka kisha amfurahishe mumewe.
Jocelyn Wildenstein ambaye ni maarufu kwa jina la Catwomen, mwenye uraia wa nchini Marekani alifanya upasuaji wa sura mara 24 akijaribu kutengeneza uso wake ufanane na wa paka.
Jocelyn alifanya yote hayo kujaribu kumfurahisha mumewe, Bilionea Alec Wildenstein aliyekuwa na mapenzi mkubwa kwa paka.
Kwa kumtazama usoni, Jocelyn amebadilika na muonekano wa sura yake haupo kama binadamu wa kawaida. Hali hiyo ndiyo iliyomfanya ajulikane kama Catwomen.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment