Wizara ya Afya Tanzania imesema sasa hivi kila Mtu anayeingia kwenye chombo cha usafiri wa umma lazima awe amevaa barakoa (mask) kama ilivyoelekezwa kwenye mwongozo isipokuwa Watoto wenye umri wa chini ya miaka 8 tu.Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Makubi amesema pia ———> "Wasafiri wawezeshwe kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka kabla ya kuingia kwenye vyombo vya usafiri hivyo, viongozi wa mtaa husika wahakikishe kuna vyombo vya kuhifadhia maji na sabuni vya kutosha katika kila kituo"
"Abiria wote waendelee kuelimishwa kuhusu umuhimu wa kutosongamana ndani ya vituo vya Mabasi kupitia walinzi getini, wahudumu wa mabasi na askari wa usalama wa barabarani, aidha boda boda wabebe kwa idadi sahihi (1-2) (siyo mishikaki) na wavae barakoa" ——— Prof. Makubi.

0 comments:
Post a Comment