Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Friday, July 16, 2021

WAZIRI MKUU MTEULE WA LEBANON AJIUZULU

 

Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Saad Hariri ametangaza kujiuzlu baada ya kushindwa kuunda serikali kwa karibu miezi tisa.

Hariri ametangaza uamuzi wake huo baada ya kukutana na Rais Michel Aoun. Amesema wameshindwa kufikia makubaliano.

Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Saad Hariri amesema Rais Aoun alikuwa ametaka marekebisho yafanyike kwenye safu ya mawaziri aliowapendekeza. Mwanasiasa huyo amesema wamejadili mambo yanayohusiana na uaminifu, na ni wazi kuwa hakuna chochote kilichobadilika.

Serikali ya Lebanon ilijiuzulu baada ya mlipuko mkubwa ambao ulitokea kwenye bandari ya Beirut mnamo Agosti 4 lakini imeendelea kufanya kazi katika hadhi ya serikali ya mpito.


0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates