Naingiza mikono mfukoni,Naanza na ya mbele upande wa kushoto,nahama Nahamia upande wa kulia HAKUNA!...
Mifuko ya nyuma nakumbuka nishaweka Wallet kushoto ,kulia Nishaweka Kitambaa cha kujifutia jasho kutokana na Harakati na jua la Dar!
Nitaipata wapi! Au Nikanunue? Na je Nitaipata kweli KALAMU ambayo nitaanza Moja mpaka Mwisho kumuandika mtoto wa YESSAYAH pasipo kunigomea njiani?
Nawaza nitaipata wapi kalamu yakuandika mambo makubwa aliyoyafanya mtu Huyu Kwenye Game la Muziki wa Bongo Hasa HIP HOP!
Kwa kua Mmoja ya Wasanii wa Mwanzoni kabisa Nchini wa HIP HOP waliofanikiwa kuipunguza makali ile kauli ya “HIP HOP YA BONGO HAILIPI “
Mpaka leo hii Tunamtolea mfano yeye Na binamu yetu kabisa @mwanafa N.k!
Msanii wa Mwanzoni kabisa kutambua na kujua thamani ya BRAND! Na kuitafuta thamani yake pasipo Matumizi ya KIKI ama Bifu! Huyu alijua maana ya Brand na alijua namna nzuri yakuitengeneza pasipo kuja kujilaumu baadae...
Kizazi hiki cha muziki wa sasa kina cha kujifunza hapa!
Natamani kumuandika,Natamani sanaa mkumbuke ...
Huyu ndo Msanii wa Mwanzoni kabisa kula deals kubwa kubwa wenyewe sikuizi mnaita (Endorsements)na Makampuni Makubwa Mbalimbali nchini...
Ndo huyu mwenye Tuzo ya Channel 0 ndani ,Naikumbuka ile ya 2012,Hapo nikizitoa tuzo kibao za ndani ya nchi .. kumbuka ni Mwana HIP HOP huyu π
Natamani mashabiki wa sasaivi wajue AY ni nani? Na Amefanya yapi,Ijapokua yeye mwenyewe sio mzungumzaji sanaa Wa Ushindi wake wote huu ..
Nadhani alijua fika hiyo ndo kazi ya watu kama sisi,Washika kalamu kwa ajili ya Kuiandikia Jamii Mambo Makubwa Wafanyao Watu katika maisha yakila siku...ili Wasi ishie tu kuburudika bali wajifunze piaπ..
Ubaya sasa Nishakua Mzembe wa kazi,Kalamu hiyo Sina Na Sina uwezo wa kuipata kwa sasa π£
Hakika @aytanzania Huna Deni Kwenye kuchonga Njia ambayo Sote ni mashuhuda,kizazi cha leo tunaona inavyowalipa Haswaa .

0 comments:
Post a Comment