Mkuu wa wilaya wa Njombe, Mh. Kissa Kasongwa amezindua rasmi Mbolea iitwayo HAKIKA, mkoani Njombe. Mbolea hiyo imethibitishwa kwa ubora na TBS, TFRA na kimataifa kwa matumizi ya kilimo cha parachichi.
Mbolea ya HAKIKA inazalishwa na Kiwanda cha Guavay kilichopo jijini Dar es Salaam inamuwezesha mkulima kuuza parachichi nchi za ulaya na marekani.
Uzinduzi huo umeudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo, Wizara ya Kilimo, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), TAHA, Chuo cha Kilimo cha Sokoine, SAGCOT, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Tume ya Taifa ya Sayansi na Tekinolojia,COSTECH.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) Pro. Anthony Mshadete, ame eleza kwamba uzinduzi wa mbolea ya Hakika umekuja wakati muafaka ili kuongeza matumizi ya mbolea nchini na tija ya uzalishaji wa zao la parachichi linalo kizi viwango vya soko la kimataifa (export market).
Hata hivyo Mkurugenzi wa kampuni za mbolea ya Eng. Ahad Katera amewasihi wakulima kuchangamkia fursa hii kwani mbolea hizo tayari zimesha sambazwa kwa mawakala wa pembejeo katika mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya , Songwe, Ruvuma, Kilimanjaro na Arusha.

0 comments:
Post a Comment