Friday, July 16, 2021
VURUGU YA AFRIKA KUSI YAATHIRI MALI ZA WAGENI AKIWEMO MTANZANIA OMMY. 4K.
Mtanzania Omary Juma maarufu @ommy.4k, Mwandishi wa Habari na Mjasiriamali anayefanya kazi Afrika Kusini akiendesha kipindi cha ‘Kutoka Ughaibuni’ ni miongoni mwa waliothiriwa na vurugu zinazoendelea Afrika Kusini baada ya Ofisi yake kuteketezwa kwa moto na vifaa vyote ndani yake Jijini Johannesburg.
“Ofisi yetu ambayo nina shea na Raia wa Cameroon Alino Alino ilikuwa inahusika na production (kuandaa vipindi vya TV na picha), kutengeneza mashine za kukandamizia makopo na takataka nyingine kuzifanya kuwa ndogo kwa ajili ya kutunza mazingira”
Omary ambae amepata hasara ya Tsh. milioni 321 alikua mbali kikazi kutokana na Ofisi yake hiyo ambayo iliaminiwa na wengi mpaka kufanya kazi ya kupiga picha Ubalozi wa Tanzania, kwa Chakachaka na kwenye mikutano ya Rais mstaafu Jacob Zuma na Rais wa sasa Cyrill Ramaphosa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment