Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Monday, July 12, 2021

UTAWALA WA CHAMA CHINA NI KAMA TANZANIA.

 


Chama cha kikomunisti
 ni chama cha kisiasa kinacholenga kufikisha jamii katika hali ya ukomunisti yaani jamii bila matabaka ya matajiri na maskini na bila watu wenye mali nyingi kuliko wengine. Katika nadharia hali hii ya ukomunisti imedhaniwa kuwa bila utawala wa watu juu ya wengine lakini nadharia hii inadai pia ya kwamba kuna kipindi cha mpito ambako chama cha kikomunisti kinatawala kwa namna ya kidikteta hadi mabaki ya utaratibu wa kale yamekwisha ambayo yanaweza kuzuia au kuchelewesha maendeleo ya kuelekea ukomunisti.

Vyama vya Wakomunisti vilifaulu kushika serikali katika Urusi tangu 1917, katika Umoja wa Kisovyeti tangu mnamo 1920 / 1924 halafu katika nchi za Ulaya ya Mashariki tangu 1945 / 46. Katika China, Korea ya Kaskazini na Vietnam ya Kaskazini Wakomunisti walitawala tangu mnamo 1948 /49. Vyama mbalimbali katika nchi kadhaa za Afrika vilifuata mtindo wa Wakomunisti kwa namna fulani na kushika utawala kwa miaka kadhaa.

Utawala wa vyama vya kikomunisti uliporomoka mnamo 1989 katika nchi nyingi na leo hii (2011) vyama vya kikomunisti vinatawala katika nchi chache pekee kama vile ChinaVietnam na Kuba. Lakini havilengi tena kufikia shabaha ya ukomunisti.Tangu mwaka 1949 mpaka leo hii hakuna chama cha siasa kutokea nchini china kimewahi kuweza kukitoa mdarakani chama cha kikomunisti, bila ya kusahau china ina watu zaidi ya bilioni 1.3 na ndio nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani.

   


0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates