MAKALA KUHUSU JAMII NA UNYANYASAJI KWA WATOTO .
maeneo
tofauti tofauti, lakini leo nataka kuangalia zaidi katika majumba ambayo Watoto
wanaishi na baba wakambo au Watoto wanaoishi na mama wakufikia maarufu mama
wakambo.
Ndani
ya jamii zetu husika tunazo ishi zinachangamoto nyingi za unyanyasaji wa
kijinsia katika Unyanyasaji ni nini?. Ni hali ya kumnyima mtu, haki zake za
msingi au kumbagua kutoka kwenye usawa na haki kumleta kwenye udhalilishaji.
Kuna jamii nyingi zinasemaga na kutumia neno unyanyasaji lakini hawatambui
maana yake, mfano unaishi na mtoto wa kufikia anatakiwa aende shule akiwa msafi
kama umri wake ukiwa bado haezi kujiandaa mwenyewe lazima apate msaada wa
mkubwa wake au akirudi shule kabla ya kuendelea na majukumu mengine lazima
kwanza apate chakula na muda wa kupumzika ili mwili upate nguvu lakini kwenye
baadhi ya nyumba haipo hivyo unakuta mtoto anafanyishwa kazi juu kazi hata kama
amerudi shule muda huo huo.
Tukiaangalia matukio mengi yanayoendelea na kunyamaziwa katika jamii zetu ambazo zina wafanya watendewa wapitie wakati mgumu katika Maisha yao hasa mabinti zenu kwa sababu watu wanaoshuhudia matendo hayo wanakosa ujasiri wa kusogea mahala husika na kutoa taarifa kwa wakati mfano, polisi, ustawi wa jamii, serikali za mitaa na wajumbe wa mitaa. Lakini ukifuatilia kwa undani Zaidi kuna jambo linaitwa vitisho vya kimya kimya kwa shuhuda aliyeshuhudia tukio hilo na mhusika mara nyingi vitisho kali huwa ni kupotezewa uhai au kuhamishwa makazi yao wanayoishi, serikali inatumia nguvu kubwa kuchunguza kesi za unyanyasaji wa kijinsia kwenye jamii zetu na kukosa Ushahidi wa kutosha kwa kuwa watendaji wanakipato cha kupoteza Ushahidi kwa wakati kwenye nyumba nyingi za maeneo ya mjini kama Dar es salaam na Zanzibar tunaona Watoto wa kiume kwa wakike wakilawitiwa na baba zao wakufikia lakini hakuna hatua yoyote ya kisheria wala adhabu kali kuchukuliwa na vyombo vya usalama kwa kuwa hakuna Ushahidi wa uwakika, bila kusahau tunaona maeneo ya vijijini wakina mama wanaoishi na Watoto wa kufikia wanavyowatesa kwa kunyoma na moto wakikosea bado haitoshi wanawachana na vitu vya ncha kali sehemu za siri wakifanya makosa pia kuna mpaka wababa halali baadhi nao wanafanya vitu vya kijinga na kikatili kwa Watoto wao waliowazaa wenyewe.SERIKALI HII INAPINGA UNYANYASAJI.
Mfano mdogo kutokea nchini Marekani, Mwaka
2017’’ Vanessa Jackson Raia wa Marekani alipogundua kuwa mume wake aitwae
``Vicent Philiph’’ amembaka mtoto wake wa miaka 7 alijichukulia sheria mkononi,
alitegea mume wake amelala kisha akamwagia petrol na kumuwasha moto alipo
kamatwa na polisi aliulizwa kwanini alifanya hivyo aliwajibu ‘’ kumpiga risasi
ingekuwa bado nimemtendea wema sana.
Tunahitaji
kupaza sauti kwa jamii ili kufikia lengo la kupinga ukatili na unyanyasaji wa
kijinsia.
PAZA SAUTI TOKOMEZA UNYANYASAJI.


0 comments:
Post a Comment