
Baadhi ya vilabu vya usiku huko England vimeanza kuhitaji pasi ya kuonesha hali ya mtu ya corona ili kuingia huku wabunge wakijadili matumizi ya pasi hizo.
Pasi hizo za Covid zilizoidhinishwa na wizara ya afya zinaruhusu watumiaji kuonyesha uthibitisho wa chanjo waliopata, vipimo walivyofanyiwa au hali ya kinga yao mwilini wanapotaka kuingia kwenye kumbi.
Pasi hizo zinapatikana kupitia programu ya kwenye simu kutoka wizara ya afya Uingereza, ambayo ni tofauti na programu ya Covid-19 huko England na Wales.Mawaziri walikuwa wameombwa kufutilia mbali pasi hizo au watoe fursa kwa wabunge kijadili suala hilo bungeni.
Msemaji wa maswala ya ndani ya nchi wa chama cha Liberal Democrat Alistair Carmichael aliwashutumu mawaziri kwa kutoa hakikisho la matumizi ya pasi hizo."Sasa tuna kitambulisho kipya kilichopo kwenye simu zetu bila hata kunongona, kutoka kwa serikali", alisema.
Waziri Mkuu Boris Johnson alitangaza mapema mwezi huu kwamba watu wanaohudhuria vilabu vya usiku na kumbi zingine kubwa ambapo umati wa watu hukusanyika watahitajika kupatiwa chanjo kamili kuanzia mwisho wa mwezi Septemba.
Wamiliki wengine wa vilabu vya usiku hapo awali waliambia BBC kwamba pasi hizo za Covid zilikuwa "hazitekelezeki" na kwamba hawatazihitaji.
0 comments:
Post a Comment