Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, July 20, 2021

TUNU HASSAN: UZEE WANGU UTAFANA SANA.


Kama Jalaal akinihuisha mpaka niotaopo manywele Meupe, Basi nitawasimulia wajukuu zangu juu ya Talanta niliyowahi kuitia machoni enzi za uhai wa Mboni Zangu. Sitowaficha kitu, nitawaeleza juu ya mmiliki wa talanta hiyo yenye kupambwa na sauti maridhawa, si mwinngine huyu.. ni wewe Tunu Bint Hassan Bin Shenkome.

Halikumithilika kamwe lile tabasamu la siku ya 19  julai kwenye kinywa cha Bi Mariam Shaaban (Mwenyezi Mungu Amrehemu) katika hospitali ya Ebrahim Haji hapa Dar es salaam, tabasamu lile lililetwa nawe pale ulipozaliwa. Urembo uliyokithiri na nuru iliyotukuka vilitosha sana kuangaza koo za Baba na Mama.
.
Kabla sijaendelea, nikujuze tu, Ninalo furushi nililopewa na Wanamichezo kukutunuku wewe Tunu, kabla ya yote nikusalimu kikwenu "Honga?" Bila shaka utanijibu "iweedii".Heri na fanaka zizidi kukuangukia Binti wa kisambaa Mwenye kujuzu Haiba na tajiriba kwani licha ya lila na Fila, ukakishika kijiti.
.
Licha ya kuwa kwenye jamii imfunzayo mtoto wa kiume kuomba radhi kwa makosa yake, huku ikimsihi wa kike kuomba radhi kwa madhaifu yake, wewe ukakaiuka kasumba hii. Kisha ukayaenzi matamshi ya Mtumbuizaji mmoja wa marekani ya mbali Bwn. Charles Malik aliyesema.
.
The fastest way to change society is to mobilize the women of the world, yani njia haraka ya kuibadilisha jamii ni kumtumia mwanamke. Swadakta!.
! Ukaitambua thamani yako kisha ukaivalia njuga sekta hii ya michezo, leo hii , ni nani asiyetambua Talanta na uwezo wako katika tasnia ya habari?
.
Leo hii wasichana wenye ndoto za utangazaji, wanakutazama wewe kama ulivyowatazama kina Zuhura Yunus na Godwin Gondwe enzi zako za mafunzo. Ninalo Furushi la zawadi kutoka kwa wanazengo, furushi hili limejaa pongezi na Dua juu yako.
.
Tunu sasa naweza kukufungulia Furushi hili. Naam, hizi ni salamu za heri ya uzawa wako.🍫💝💖⚘

Heri ya siku ya kuzaliwa ewe mrembo wa tabia na maumbile. Umetukuka mno tunu, kila ukisogeleacho hutukuka pia. Nitamaliza tenzi na Nahau kukusifu kwa vizazi na vizazi kama Nitauona Uzee wangu, hakika uzee wangu utafana sana.
.
May this day be as sunny as your smile, and as beautiful as you are.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates