Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, July 20, 2021

MWIGULU NCHEMBA AWEKA WAZI TOZO YA MSHIKAMANO.

  


“Ile tozo ambayo Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anaiita 'Tozo za Mshikamano' dhamira yake ilikuwa Serikali kuanza safari ya kujenga Barabara za lami Vijijini hili jambo ukikaa huku Dar es Salaam unaweza kuliona kama dogo lakini Vijijini huko hakuna Barabara”


“Songea kuna kijiji ambacho kuna sehemu hakuna mawasiliano ya Barabara TANROADS waliweka lami ya kawaida sana tena sehemu korofi, huwezi amini inapofika Saa 11 jioni wanakijiji wote wanakaa pale ndio sehemu yenye staha, ndio sehemu yao ya kutalii"

“Serikali imeamua kuanza kujenga Barabara za lami vijijini, wakaamua kuweka tozo ya mshikamano ili kupanua wigo wa tozo kwahiyo hii tozo imelenga kwenye eneo hilo"

“Serikali ilikusudia kwenye tozo ya miamala na ile ya laini za simu palikuwa panatarajiwa karibu Trilioni 1.6 na Trilion 1 zilikuwa zinatakiwa zitoke kwenye miamala, hizi tozo zilitakiwa ziende zikajenge Barabara na vituo vya afya vijijini”———Msemaji Mkuu wa Serikali @gersonmsigwa kwenye Clouds360 ya @cloudstv

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates