Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, July 20, 2021

SELOUS KWENYE URITHI WA DUNIA.

 


 Tanzania imeshinda katika utetezi wake kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambalo lilitaka kuliondoa Pori la Akiba la Selous katika orodha ya Urithi wa Dunia kutokana na kutekelezwa kwa mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere katika mto Rufiji (Stiegler’s Gorge).

Pori la Akiba la Selous litabaki katika orodha ya urithi wa Dunia na mradi wa kuzalisha megawati 2,115 unaoendelea kwa sasa umefikia 54% na utakamilika Juni 2022
huku ukichukua eneo dogo la asilimia 1.8 tu ya Pori zima la Selous.

Mkutano wa UNESCO unaofanyika China, huku Tanzania ikihudhuria kwa Njia ya Mtandao

Miongoni mwa sababau zilizoainishwa kuhatarisha kuondolewa kwa Pori la Akiba la Selous katika orodha ya Maajabu 1,121 ya Dunia ni kuwepo wa Ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere likitajwa kuwa chanzo cha kutoweka kwa BAIONUWAI kwenye eneo hilo.

Tanzania ni Mwanachama wa UNESCO tangu Mwaka 1962 huku Maeneo Saba Nchini ambayo ni Hifadhi za Ngorongoro,Serengeti, Kilimanjaro, Pori la Akiba Selous, Michoro ya Miambani Kondoa, Mji Mkongwe wa Zanzibar, Magofu ya Kilwa Kisiwani na Magofu ya Songo Mnara yakitambuliwa kama Maeneo ya Urithi wa Dunia.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates