Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Wednesday, July 28, 2021

RAIS SAMIA ACHANJWA LEO KWENYE UZINDUZI WA CHANJO TANZANIA.


 Leo tunazindua uchanjaji Tanzania tukijua chanjo ni ndogo ukilinganisha na idadi ya Watu, kama alivyosema Waziri wapo wanaozikataa lakini wanaozitaka ni wengi sana, nina meseji nyingi Watu wakiuliza Mama chanjo lini chanjo lini?” ——— asema Rais Samia Ikulu DSM leo akizindua uchanjaji chanjo ya corona Tanzania.

“Niwahakikishie Watanzania wale wote ambao kwa hiari yao wapo tayari kuchanjwa tutahakikisha chanjo zinapatikana, chanjo ni hiari ya Mtu lakini pia chanjo ni imani, mwilini mwangu hii chanjo ya leo ni ya sita, tulichanjwa tangu nikiwa Shule ya Msingi na zimenipa uzima wa kutosha mpaka leo nipo hapa”

“Wakati ule tukiwa tunachanja wapo Wazee walikataza lakini Shuleni tulilazimishwa tukachanja, yapo madhara kuna waliovimba mikono mpaka leo wana makovu lakini tulichomwa” ——— Rais Samia.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates