Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Wednesday, July 28, 2021

HAJI MANARA ATOA NENO.


 Aliyekuwa Msemaji wa Simba, @hajismanara amefunguka kuwa NENO lake ni moja tu baada ya uongozi wa timu hiyo kutoa taarifa ya kuachana nae leo Julai 28, 2021.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, #Manara amepost picha akiwa ameshika begi akitembea na kuandika neno kubwa kwake ni Alhamdulillah akimaanisha anamshukuru Mungu.

"Kila tunapomaliza Mechi yoyote ile ya Simba, neno langu la kwanza baada ya matokeo yoyote yale ni Alhamdulillah.

Kwa wanaofuatilia page hii wanatambua hilo. Kwangu neno hili ndio Msamiati ninaoutumia mara nyingi zaidi na hufanya hivi kwa kila jambo, liwe jema au baya. Yes neno langu ni moja tu
 AL-HAMDULILLAH" - alimalizia @hajismanara.

Kwa mujibu wa taarifa ya Simba leo, nafasi ya Manara imezibwa na mwanahabari Ezekiel Kamwaga ambaye atakaimu kwa miezi miwili.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates