Ujumbe wa 50 ulisomeka "Nimempoteza Pop (Smoke) kabla hajapata nafasi, huyu (Da Baby) tayari ameshatoboa, nitamfundisha kila kosa nililofanya ili asirudie hayo na aje kuwa bora zaidi yangu. Hii ni HIP HOP"
#DaBaby na 50 walikutana mapema wiki hii katika mitaa ya New York, na Rapa huyo chipukizi hakusita kuonesha shauku yake ya kuonana na 50 Cent, alipoandika kupitia ukurasa wake wa Instagram post iliyosomeka, "Mtu ambae nimekuwa nikimtazama muda wote tangu naanza, ameniazima saa chache katika muda wake leo, waliokuwa wanaogopa kunipa nafasi wamejichanganya na kujikuta wananipa nafasi ya kukutana na 50 Cent, kosa kubwa sana hilo"
#DaBaby anajiandaa kutoa album yake, na tayari ameshaweka vionjo viwili nje, ngoma ya "Ball If I Want To" na "Red Light Green Light" na ya tatu ikiwa njiani inakuja.

0 comments:
Post a Comment