Mbunge wa Muheza Mh. Hamis Mwinjuma (@Mwana FA ) ameendelea na ziara ya kuwashukuru Wananchi kwenye Kata mbalimbali, Na kufanikiwa kufanya yafuatayo.1. Amefika na kushirikiana na wananchi katika msalagambo kufanikisha Mradi wa kupeleka maji kata ya Pande Darajani ambapo kwa sasa hatua iliyopo ni kulaza mabomba toka kwenye Tanki lililopo Muheza (ya Jimbo la Tanga) kuelekea kijiji cha Darajani.
2. Mbunge @MwanaFA ameshiriki pia ujenzi wa Madarasa mawili ya Shule ya msingi Kwamkabala ambapo hatua iliyofikiwa leo ni kuwekwa Jamvi, ikumbukwe Madarasa haya yalikua miongoni mwa ahadi za @MwanaFA alizotoa kwa Wananchi kwenye Uchaguzi uliopita na alishawezesha kukamilika kwa darasa moja kwenye shule hiyo ambayo awali ilikuwa na vyumba vitatu tu vya madarasa vilivyofanya watoto wa darasa la nne kulazimika kuhamia katika shule ya msingi Masuguru ili kuendelea na masomo yao.
3. Mbunge @MwanaFA amefanikiwa kufanya mkutano wa Shukrani kwenye kata ya Mbaramo iliyopo Jimbo la Muheza ambapo aliutumia kuwapa mrejesho wa changamoto mbalimbali za Kata hiyo alizozishughulikia kufikia leo.
Hizi ni ziara ambazo Mbunge wa Muheza anazifanya kwa sasa Jimboni ili kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni zinakamilika kwa Wananchi wa Muheza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment