AMENORRHEA
Ni hali ya mwanamke ambaye amepevuka na kukomaa maumbile yake ya uzazi kushindwa kupata hedhi /kupitiliza siku za hedhi.
Kwa ufupi tatizo hili limekua likiwakumba na kuwaletea usumbufu wa kisaikolojia wanawake wengi wakidhani kwamba wamepata ujauzito nk. Hata hivyo tatizo hili la kukosa hedhi linaweza kutokea awali(primary) au baadae maishani (secondary).
AINA ZA AMENORRHEA (KUKOSA HEDHI)
1.Primary Amenorrhea.... Hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke /msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo ambapo hali hii huweza kuendana na kutopata mabadiliko yanayoambatana na kuvunja ungo kama vile kuota nywele sehemu za siri, kuota matiti nk ila bado hapati siku zake.
Hii husababishwa na:-
1. Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwenye via vya uzazi.
2. Kuziba kwa utando unaozunguka uke (Hymen) hivo kukosekana tundu la kupitisha damu (Imperforate hymen)
3. Utapiamlo
4.Sababu za kimaumbile kama vile kuzaliwa bila kizazi au kukosekana kwa uke nk.
SECONDARY AMENORRHEA....
Hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito wala hanyonyeshi na ambaye hajakoma hedhi ambapo awali alikua akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa muda huenda ni miezi au mwaka mzima hapati hedhi mpaka sasa.
Hii husababishwa na :-
1. Madawa.. Kwa mfano dawa za uzazi wa mpango, dawa za pressure, dawa za cancer nk.
2. Uzito mdogo kupita kiasi
3.Msongo wa mawazo
4.Magonjwa mbalimbali
5.Mazoezi.. Kwa mfano wale wanaokimbia umbali mrefu nk
6.Vyakula tunavokula
7.Mazingira nk
PHYSIOLOGICAL AMENORRHEA.....
Hii ni hali ya kawaida ya kawaida ya mwanamke kukosa hedhi ni kama ujauzito, kukoma kwa hedhi (menopause), na kwa wale wasichana ambao bado hawajafikia umri wa kubalehe
DALILI ZA KUKOSA HEDHI (AMENORRHEA)
1.Mwanamke kuwa na vinyweleo vingi na kuota ndevu hii inamaanisha ni kiashiria kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni za kiume za androgen
2.Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito wala hanyonyeshi
3.Uke kuwa mkavu
4.kwa wale wasichana ambao wapo kwenye umri wa kubalehe Lakini haikuwa kunakua na Ukosefu wa kiwango kikubwa cha homoni iitwayo testosteroni
5.kuumwa na kichwa
6.Mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria kuwepo kwa tatizo katika ovaries.

0 comments:
Post a Comment