Tuesday, July 20, 2021
MISS TANZANIA AMETOA TAMKO KUHUSU BASATA.
Baada ya kamati ya Miss Tanzania kuanika makosa sita yaliyomtia hatiani Miss Tanzania, Rose Manfere na kumuengua kushiriki shindano la Miss World, leo Kamati hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram imeeleza kile kilichoiita elimu kwa wadau ikikazia kuwa hakuna aliyejuu ya Sheria.
Kwenye maelezo hayo, Miss Tanzania pia imelitaka Baraza la Sanaa Taifa (Basata) wasimamie misingi ya Sheria na Kanuni ili wawe salama.
"ELIMU KWA WADAU WETU inaendelea..🇹🇿👑
Mungu hadhihakiwi. Hata Yesu Kristu alisulibiwa msalabani na dunia nzima kumgeuka ila watu wema walikua nae na Mungu mwenyezi na ushindi ukawa kwake.
Kwahiyo kwa sababu Pilato alisema asulubiwe basi mamlaka ilikua sahihi? Wote mmaujua ukweli. Hivi watu makini hawajiulizi .Mbona mshindi wa kwanza alishinda, pili The Look ilishawekeza Kwake , sasa kama hasara ni ya nani? Iweje waanze upya kuwekeza kwa mtu mwingine?.
Ni kwa sababu tunajukumu kubwa la kumpeleka mtu anaewakilisha TANZANIA nzima. Dhambi ya kumpeleka mtu aliyeonyesha KUKOSA sifa ya uwakilishi wa nchi na lana yake tutaibeba sisi ( ilihali tulizigundua kasoro mapema) ndio maana Sheria na kanuni ziliwekwa ikitokea tatizo kubwa kama hilo kamati inapaswa kuchukua hatua gani? Tumetekeleza . kamati imeenda mbele kupunguza makali ya adhabu kama kuweka 'pending' swala la kumvua kabisa taji na kumnyanganya zawadi ili kumpa nafasi ya kujitafakari na kujifunza. Na ikishindikana ndio ikamilishe adhabu hiyo.
Tunatimiza wajibu wetu kikamilifu 🙏 Sisi tunasonga mbele na watanzania makini !!
Kazi zinaendelea.
NO ONE IS ABOVE THE LAW
BASATA wasimamie misingi ya SHERIA na KANUNI
watakua salama. Haki isipopatikana BASATA itapatikana MAHAKAMANI
With Tanzania representative @juliana_rugumisa usikose kumfuatilia leo akiendelea na majukumu yake ya 'Beauty with a purpose' Huyu binti anatushangaza na uchapaji kazi wake. Tunamuombea na anaenda kuishangaza dunia @juliana_rugumisa THE NEW FACE OF AFRICA FROM TANZANIA TO THE WORLD
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment