Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Friday, July 30, 2021

MHE. GEKUL ATOA RAI KWA TFF KUTOA ELIMU KWA WACHEZAJI NA VILABU KUHUSU MAWAKALA.







 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul ametoa rai kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kutoa elimu kuhusu mawakala wa michezo na kwa siku za usoni itengeneze kanuni zitakazowasimamia mawakala hao.

Mhe.Gekul ametoa rai hiyo Julai 30 alipofungua Kongamano la wadau wa mpira wa miguu (Tanzania Football Summit 2021) linalofanyika kwa siku mbili Jijini Da er Salaam ambapo amesema
ni vizuri wachezaji wote na vilabu kutumia mawakala pale wanaposajili wachezaji.

"Tanzania mpaka karne hii tuna mawakala takribani 6 tu nchi nzima ambao wanatambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ikiwemo AFRISOCCER Kampuni iliyoandaa kongamano hili, Idadi hii ni ndogo sana hairidhishi na hii inamaanisha wachezaji na wadau wa soka bado hawajafahamu umuhimu wa kutumia mawakala katika soka" amesema Mhe.Gekul

Naibu Waziri Gekul ameongeza kuwa Dunia ya sasa inakwenda kidijitali wachezaji wanauzwa na kutafutiwa timu kwa kutumia tovuti (Websites) na mifumo mbalimbali, pia taarifa za vilabu, wachezaji, makocha na mawakala katika ulimwengu wa sasa zinahifadhiwa kidijitali, Wachezaji wa kisasa wanafuata ratiba za mazoezi, aina za mazoezi na vyakula kidijitali. Hivyo ni wakati sasa nchi yetu kukimbizana na ulimwengu wa teknolojia hiyo.

"Matumizi ya mawakala yatapunguza kama sio kuondoa migogoro ya kunyang’anyana wachezaji kabla ya mikataba baina ya vilabu, Pia itapunguza migogoro kati ya wachezaji na vilabu kwakuwa pale unapotokea mgogoro kati ya mchezaji na klabu, klabu itawasiliana na wakala wa mchezaji husika badala ya kuwasiliana moja kwa moja na mchezaji. Pia mchezaji atapata muda wa kuendeleza kipaji chake badala ya kuwaza kujitafutia timu au kusuluhisha migogoro kati yake na klabu"amesisitizs Mhe.Gekul.


0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates