Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Saturday, July 31, 2021

KINDA WA AJAX AFARIKI DUNIA


 Kinda wa klabu ya @Afcajax Noah Gesser mwenye umri wa miaka 16 amefariki usiku wa kuamkia leo kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata kwenye ajali ya gari iliyotokea jijini Amsterdam, Uholanzi


Gesser alikuwa mmoja wa abiria waliokuwepo kwenye gari (taxi) ilioyopata ajali mbaya, abiria mwingine aliyekuwepo kwenye gari hilo alipoteza maisha hapo hapo, Dereva wa gari hilo amekimbizwa hospital na anaendelea na matibabu. Lakini chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

Kinda huyo alijiunga na Ajax 2018, alikuwa anasifika kuwa hatari anapokuwa mbele ya lango la timu pinzani. Katika michezo yake sita ya ligi ya vijana wenye umri chini ya miaka 16 ambayo bado inaendelea amefunga mabao 11.
#RipGesser🙏

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates