unaposema hatuna kikosi kipana, sikuelewi. Tumekuwa na timu nzuri msimu huu . Vijana wamepambana vyema na sisi kama viongozi, wanachama na wapenzi wa timu hii..tunajivunia jitihada zao”“ tutafanya usajili mzuri kwa maelekezo ya kocha ili kuendelea kuisuka vyema timu yetu. Msimu huu tulikuwa WASHINDANI ila msimu ujao tutakuwa WASHINDI . Tumefika nafasi ya pili ligi kuu Tanzania bara, fainali ASFC na ubingwa Mapinduzi Cup. Itoshe kusema tulikuwa katika build up nzuri kuanzia wachezaji na benchi la ufundi “
“ soka lina njia zake katika kulijenga kwa maana ya kutengeneza timu ya ushindi na klabu ya mafanikio. Nina imani kwa kudra za mwenyezi Mungu , ushirikiano wetu sote; viongozi na wanachama, msimu ujao tutakuwa na timu nzuri ya USHINDI pia maendeleo ya KLABU yetu kwa michakato ya mabadiliko inayoendelea “
“ wapenzi, mashabiki na wanachama wetu wasiwe wanyonge bali wajione wapo katika njia nzuri ya mafanikio ambayo inajengwa vyema ili kuleta matunda mazuri kwa muda mrefu ujao”
Eng. Hersi Said, makamu mwenyekiti kamati ya mashindano Yanga SC

0 comments:
Post a Comment