Mawaziri wa fedha kutoka kundi la mataifa 20 yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi kote ulimwenguni G20, jana waliidhinisha mkataba wa kihistoria wa kubadilisha mfumo wa kuyatoza ushuru mashirika ya kimataifa na kuzihimza nchi ambazo hazikushiriki kujiunga katika mkataba huo. Mageuzi hayo yanayojumuisha ushuru wa kiwango cha chini cha asilimia 15 kwa mashirika ya kimataifa, yalikubaliwa na mataifa 131 mapema mwezi huu. Lakini kuidhinishwa kwa mageuzi hayo na mataifa 19 yalioimarika zaidi kiuchumi pamoja na Umoja wa Ulaya kutasaidia kuhakikisha yanaanza kutekelezwa baada ya miaka mingi ya majadiliano. Katika taarifa ya mwisho iliyotolewa na mawaziri hao baada ya mkutano wa siku mbili uliondaliwa mjini Venice na Italia inayoshikilia urais wa kundi hilo la G20, wamesema kuwa wameafikia makubaliano ya kihistoria kuhusu mfumo thabiti na bora zaidi utakaosimamia ushuru wa kimataifa.
.
0 comments:
Post a Comment