Tuesday, July 13, 2021
DAR ES SALAAM; MKUU WA WILAYA YA KIGAMBONI FATUMA NYANGASA KAWATAKA ABIRIA WA KIVUKONI KUACHIANA NAFASI.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatmah Nyangasa @fatmanyangassa amewakumbusha Wananchi wa Kigamboni kuzingatia miongozo ya kujikinga na kirusi corona kinachosababisha ugonjwa wa COVID-19 kwa kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka.
DC Nyangasa ametoa hamasa hiyo leo akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Kigamboni, Dalmia Mikaya @dashian__ ambapo amewataka Wananchi wa Kigamboni ikiwemo wanaotumia Kivuko kujilinda dhidi ya kirusi corona.
"Muachiane nafasi, mkumbuke kutumia vitakasa mikono, kuvaa barakoa na kuepuka kusongamana” ——— DC Nyangasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment