Friday, August 20, 2021
RAPPER WALE ASEMA YEYE NDIO RAPPER BORA WA MUDA WOTE.
Kuna rappers wapya kibao wenye vipaji, wazamani pia wapo, ila hawa hawapewi heshima wanayostahili, wanachukuliwa poa. Kwa upande wa rappa Wale toka Marekani yeye hajataka kusubiri heshima yako, ameamua kuweka wazi kuwa yeye ndiye rapa Bora wa muda wote.
@wale anasema kwamba, anaposema kuwa yeye ni bora wa muda wote anamaanisha toka moyoni, na kazi zake zinabainisha kupitia mitindo mpaka aina ya uandishi na utamkaji.
Wale ajinadi kuwa, nyimbo zake zote zimepata (plaques) tuzo maalumu ambayo msanii hupewa na RIAA au mtandao wa kuuza na kusikiliza muziki kutokana na mafanikio ya nyimbo zake.
Una mtazamo gani juu ya hili ⁉️
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment