
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepunguza gharama za upimaji wa ugonjwa wa Uviko - 19 kutoka dola za Kimarekani 100 hadi dola 50 kwa kipimo cha RT PCR na kuondoa gharama za kipimo cha Antigen Rapit Test mipakani isipokuwa viwanja vya ndege ambapo wasafiri watalipia dola 10 tu kwa kipimo cha Antigen Rapid Test
Serikali imeshusha gharama hizo baada ya kutenga kiasi kulipia gharama hizo kwenye bajeti mwaka wa fedha 2021/2022.
Hatua hii imefikiwa kufuatia ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Kenya Mei 4, 2021 na kutoa maelekezo ya kutatuliwa kero ya vibali na upimaji wa Uviko-19 kwa abiria wanaovuka kupitia mipaka ya nchi kavu.
0 comments:
Post a Comment