Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Saturday, July 17, 2021

ZIARA YA RAIS SAMIA SULUHU NCHINI BURUNDI IKIWA AMELENGA KUKUZA UHUSIANO WA KIBIASHARA NA KIDIPLOMASIA.

 


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko nchini Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, inayolenga kuimairisha na kukuza uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia.

Samia amewasili nchini Burundi kwa mualiko wa mwenyeji wake, Rais wa nchi hiyo Evariste Ndayishimiye, akiambatana na kundi la wafanyabiashara wa Tanzania kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji kupitia mkutano wa wafanyabiashara wa nchi hizo utakaofanyika Jumamosi hii.

Rais Samia, 61 ana miezi minne madarakani wakati Ndayishimiye, 53, ana mwaka mmoja madarakani na wote wameonyesha kutaka mabadiliko ya kiuendeshaji na uchumi katika nchi zao.

Tangu aingie madarakani Rais Samia ameshatembelea Uganda na Kenya kama sehemu za kuboresha mahusiano na kutafuta suluhu ya vikwazo vya kibiashara lakini pia alihudhuria mkutano wa dharura wa nchi za SADC nchini Msumbiji.

Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kwa Rais Ndayishimiye kuitembelea baada ya kuingia madarakani, na akiwa Kigoma, magharibi mwa nchi hiyo Septemba 9, 2020, alisema: "Tanzania ni kama mama kwa Burundi kwa sababu ilitusaidia kwenye kupigania uhuru."

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates