Friday, July 23, 2021
WATAZAMAJI WATAKAOFIKA KUTZAMA FAINALI YA FA KATI SIMBA NA YANGA MJINI KIGOMA WANATAKIWA KUVAA BARAKOA.
Mkuu wa mkoa wa kigoma ,Thobias Andengenye amewataka Mashabiki wote watakaohudhuria Mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam #ASFC kati ya Simba na Yanga kuhakikisha wanachukua Tahadhari dhidi ya ugonjwa wa CORONA ikiwa ni pamoja na Kunawa mikono kabla ya kuingia uwanjani na kutumia Sanitizer
Pia, RC Thobias Andengenye amewataka watu wote watakaongia uwanjani kuvaa barakoa muda wote wa mchezo, watakaokuwa hawana barakoa watauziwa milangoni kwa bei ya Tsh 500 tu.
Mchezo Huo wa Fainali ya #ASFC Utachezwa Jumapili hii (Julai 25, 2021) katika dimba la Lake Tanganyika 🏟 Mkoani Humo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment