Soko maarufu la Marikiti mjini Mombasa nchini Kenya limepata hasara kubwa kutokana na moto ambao ulilikumba soko hilo Jumamosi usiku kuamkia Jumapili.
Wafanya biashara katika soko maarufu
la Marikiti mjini Mombasa wamepata hasara kubwa baada ya moto mkubwa
kushuhudiwa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili
Hakuna ripoti za maafa wala majeruhi
kufikia sasa huku juhudi za kuzima moto huo zikiendelea.
Magari ya zima moto kutoka kitengo
cha serikali za ugatuzi wakishirikiana na polisi wako kwenye tukio wakijaribu
kudhibiti hali.
Wakati huu ambapo kuna sharti la
kutotoka nje wakati wa usiku kwa sababu ya kuzuia maambukizi ya virusi vya
corona, baadhi ya wakaazi wa maeneo ya karibu wako nje kushuhudia moto huo na
wengine wakitoa msaada wa kudhibiti moto.
Hali hii imewalazimu maafisa wa
kushika doria nyakati hizo kuweka usalama eneo hilo pia kuepusha visa vya
uporaji kutokea kwenye baadhi ya maduka yaliyoachwa wazi kutokana na moto huo.
Haijabainika chanzo cha moto huo, na
hakuna mwenye kufahamu nini hasa ilikuwa sababu ya moto.

0 comments:
Post a Comment