Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Friday, July 16, 2021

RAPA DRAKE AKIRI KUFANYA DNA ZAIDI YA MARA 3 KWA WANAE,


 Rapper Aubrey Graham, anayetambulika kiusanii kama #Drake, ameweka wazi presha aliyokuwa nayo wakati akisubiri majibu ya DNA ya mtoto wake Adonis.


Kupitia interview aliyofanya na TIDAL, Rapper huyo mwenye asili ya Canada, aliwaambia watangazaji kuwa alikuwa katika wakati mgumu na wenye shauku ya kuwaambia mashabiki wake kuwa yule mtoto ni wake, lakini alihofu ikiwa majibu ya DNA yangekuja vinginevyo.

"Wale wataalam wakarudi kwetu na majibu kuwa DNA iliharibika wakati inapelekwa kupimwa, kwa hivyo hawawezi kuwa na uhakika wa asilimia mia kuwa yule mtoto ni wa kwangu. Kwa wakati ule nilikuwa njia panda na nimepanic, kwa kuwa sikutaka kuiambia Dunia kuwa mtoto yule ni wa kwangu, halafu ije ijulikane sio wangu" alisema Drake kwenye interview hiyo.

"Sikuwa na majibu ya uhakika mpaka ilivyokuwa imebaki wiki moja tangu album yangu itoke, ndipo nilipopata uhakika kuwa mtoto yule ni wa kwangu, na hapo ni baada ya kufanya vipimo na makampuni mengine mawili".

Adonis alizaliwa Oktoba 11, 2017. #Drake alimpata mtoto huyo na mwanadada Sophie Brussaux.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates