Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Saturday, July 17, 2021

RAIS WA FIFA GIANNI INFANTINO AWAPONGEZA TIMU YA SIMBA SC KWA KUCHUKUA UBINGWA VPL 2010/2021

 


Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino ameipongeza timu ya @simbasctanzania kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2020/2021.


Katika barua yake kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, Rais Infantino alisema ubingwa ni matokeo ya juhudi na kutekeleza majukumu kwa kila mmoja ndani ya klabu hiyo.

''Naomba uwasilishe pongezi zangu kwa kila mtu aliyehusika katika mafanikio ya Simba SC na kuwatia moyo waendelee kufanya kazi kwa moyo wa ushirikiano, ari na ushupavu,'' alisema Rais Infantino katika barua yake.

Pia alimshukuru Rais Karia na TFF kwa kuchangia maendeleo na ustawi wa mpira wa miguu katika ukanda huu na duniani kwa ujumla.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates