Miongoni mwa story ambazo zimegusa hisia za Watu wengi Weekend hii ni ya tukio la Mtu kupigwa risasi akiwa Baa Sinza kwa Remi Dar es salaam usiku wa July 17 2021.
Kijana Alex maarufu Simba amemuua kwa kumpiga risasi Kijana anayeitwa Gift na kisha na yeye akajiua kwa kujipiga risasi wakiwa kwenye Baa hiyo.
Sasa imebainika kwamba Alex alisherehekea Birthday yake June 13,2021 na cake moja ambayo ilikatwa kwenye Birthday yake siku hiyo ilikuwa na picha ya Bastola na hii inahisiwa kwamba huenda kwa Alex Bastola kilikuwa ni kitu anachokipenda

0 comments:
Post a Comment