Friday, July 23, 2021
ITENGENEZE KESHO MAPEMA ILI USIJUTIE KESHO YAKO.
Juhudi za maisha zisikufanye ukajenga historia mbaya baada ya kufa kwako. Maisha yako ya leo ndio historia njema ya kesho jitahidi uishi kwa misingi ya usawa na utu ili kesho yako iwe njema.Inatakiwa watu wajifunze kwenye maisha yao kwa uwepo wako, busara, huruma na kujituma ndio vitu pekee ambavyo vinaweza kuvutia watu wa karibu yako kutaka kukaa na wewe zaidi. Mwili wako unaweza kuharibika na usitambulike kabisa ila vitendo vyako kamwe haviwezi kufutika moyoni mwa watu.
Tujifunze kutengeneza historia njema ili ukumbukwe vyema. Maisha yetu yamegawanyika pande mbili kuna haya tunayoishi sasa na yale ambayo itaishi historia yetu baada ya kuwa mili yetu haipo tena. Dunia ipo tayari kukutunzia historia yako kama utajenga misingi mema leo.
Mitazamo chanya pekee ndio mtaji unaoweza kukupa heshima kila siku kwenye maisha yako. Jifunze kuwa wewe na wape watu nafasi ya kukuona wewe ukiwa unaishi kwenye uhalisia wako. Trust me maisha ni unyenyekevu na utu, watu wanataka utu wako na sio jina lako, jifunze kuwa wewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment