Maandamano hayo ya kuipinga serikali ya Cuba yanatajwa kuwa ni makubwa kuwahi kushuhudiwakatika miaka ya hivi karibuni.
"Marekani inasimama pamoja na watu wa Cuba wanaopigania haki zao za msingi na tunaitolea wito serikali ya Cuba kujizuia kutumia nguvu dhidi yao au kuinyamazisha sauti ya watu wa Cuba," amesema Biden.
Tamko hilo la Biden limeonyesha msimamo tofauti na wa mtangulizi wake wa chama cha Democratic Barack Obama, ambaye wakati wa uongozi wake alijaribu kupunguza mivutano kati ya Marekani na Cuba pamoja na kuilegezea nchi hiyo vikwazo ilivyokuwa imewekewa.

0 comments:
Post a Comment