Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Sunday, July 11, 2021

ASAPROCK; AWEKA WAZI UJIO WA VIDEO MPYA AKIWA NA RIHANA.

 


RAPA wa miondoko ya Hip Hop kutoka  Marekani ASAP Rocky ametangaza kwamba yupo katika mapenzi na mwanamuziki nyota wa miondoko ya Rnb  Rihanna.

Rapa huyo alimuelezea Rihanna kuwa penzi la Maisha yake katika mahojiano na GQ.

Uvumi kuhusu iwapo nyota hao wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi ulianza mapema 2013, wakati rapa huyo alipomsaidia Rihanna katika ziara yake ya Diamond World Tour.

“Yeye ni sawa na labda milioni wengine, Nadhani wakati unajua, unajua tu,” alisema. “Ni Yeye tu.”

Wawili hao walishiriki katika Video ya ASAP Rocky ya 2013 ya fashion Killa.

Tangu wawili hao walipoanza mahusiano ya kimapenzi , wamekuwa wakijaribu kuwazuia waandishi wa habari kuwapiga picha pamoja, taarifa hiyo ilisema.

Rapa huyo alisema kwamba mpenzi wake ndiye aliyeishawishi albamu yake mpya ambayo itamshirikisha Morrissey.mchana wa leo wapendanao hao wameonekana maeneo ya miami wakiwa katika pozi la kupiga picha tofauti tofauti na Asaprock amepost katika mtandao wake wa instagram akisema ``Asap rocky and Rihanna shooting a new musi video'' tukae mkao wa kula kuona ni nini kina kuja kutoka kwa wawili hao,

                    Mwandishi; F.A.Maige

                  simu no. 0657 129 225

  Wale wote wapenzi wa burudani hapa ndipo mahala pekee usikose kutembelea kila siku.Asante

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates